kufanywa na director wa Kenya aliyefanya ‘Asante’ ya AY Single mpya ya ‘Mfalme’ imemrudisha kwa nguvu Mwana FA kwenye ‘headlines’ kutokana na jinsi ilivyopokelewa vizuri toka alivyoi-perform kwa mara ya kwanza katika show ya tuzo za KTMA Jumamosi iliyopita. FA amefunguka kuwa tayari mipango ya kuifanyia video imeanza na director atakayehusika katika zoezi hilo ni Mkenya aitwaye Kevin Bosco aliyefanya video ya ‘Asante’ ya AY, lakini usitegemee kuona video ya magari au nyumba za kifahari sababu sicho anachokihitaji FA. “Bosco aliniletea script juzi concept yake yeye ilikuwa kama Mwana FA amefanikiwa kwahiyo anakuwa ana shukrani kwa Mungu lakini magari makubwa nyumba nini nini…” Alisema Mwana FA jana kupitia Kwetu Flevah ya Magic FM na Dj Tass. “Moja ya sababu ya mimi kuichagua hii beat kwanza sample za kimasai ni kwasababu nataka kufanya African Hip Hip, siwezi kushindana na kina Jay Z kwa aina yao ya muziki wanayofanya lakini naweza kufanya muziki wangu ambao ukapenya Afrika nzima kwasababu utakuwa wa kiasili wa Kikwetu. Kwahiyo nataka video ambayo itakuwa inanionesha na wamasai ikiwezekana niuoneshe mlima Kilimanjaro.
” Alisema FA. “Mimi sio mtu wa kudisplay maisha yangu na siwezi kufanya vitu feki staki kutokea kwenye ma Range sina Range, tufanye tu video ya kawaida moja ambayo concept tu tuwenayo nzuri ambayo watu wote wakiona watajua tunachozungumzia.” ‘Mfalme’ ambayo kamshirikisha G-Nako ni kama imefungua mlango kwa Mwana FA kwa mwaka huu 2014, lakini ana mpago wa kutoa nyimbo zingine mbili kabla mwaka haujaisha.
“Unajua hasira za mkizi furaha ya mvuvi , kwahiyo huu ni mwaka mzuri kwa waskilizaji na watazamaji kwa sababu kama nagadhabu, nataka watu wafurahi nimekuwa nikitoa wimbo mmoja nyimbo mbili kwa mwaka mzima. “Sasa hivi nimetoa wimbo nihesabieni wiki nane, wiki ya tisa nidaini ngoma ingine, nihesabieni tena wiki nane wiki ya tisa nidaini ngoma ingine Ramadhan ikiisha daini ngoma ingine ntawapa, ikifika mwezi wa kumi mwishoni ntawapa ngoma nyingine. “ Aliongezea, “Nina ngoma nne tano ambazo ningekuwa na uwezo ningezitoa zote kwa mwaka mmoja huu, lakini naona muda hautoshi kwahiyo pengine mtapata tatu ama nne zikizidi.
” Moja ya nyimbo anazotarajia kuzitoa baadae mwaka huu ni ile aliyomshirikisha Alikiba. Beat ya ‘Mfalme’ imetengenezwa na Nahreel huku vocals zikisimamiwa na Marco Chali katika studio ya MJ Records.
Post a Comment