0

wake Ni kama mtoto anavyozaliwa na kuanza kutambaa na baadaye kutembea, ndivyo ilivyo kwa Mkenya/Mmexico Lupita Nyong’o ambaye tumekuwa tukishuhudia mafanikio yake yakipiga hatua toka alivyoshiriki katika filamu ya ’12 Years A Slave’. Jumamosi iliyopita Lupita alikuwa miongoni mwa A-list ya watu maarufu waliopata nafasi ya kutembelea Ikulu ya Marekani katika ‘White House Correspondents Dinner’. Hiyo ilikuwa nafasi ya mshindi huyo wa tuzo za Oscar kukutana na Rais Barack Obama na mke wake Michelle Obama na kupiga picha, pia inasemekana Lupita na Obama walipata kukienzi Kiswahili katika sehemu ndogo ya mazungumzo yao.

ASANTE KWAKUTEMBELEA WEBSITE  HII JIUNGE NASI  KUWA MWANA FAMILIA WA JIMMCARTER.COM FACEBOOK-JIMCARTERTZ | TWITTER JIMMCARTERTZ

Post a Comment

 
Top