Mahakama ya Hakimu Mkazi Ilala imeiamuru kampuni ya Mawasiliano ya TIGO kuwalipa wasanii Hamis Mwinjuma 'MwanaFA' na Ambwene Yessaya 'AY' jumla ya shilingi bilioni 2.18 Fedha hizo ni za fidia baada ya kutumia nyimbo yao kama Caller Tune(Mwitikio wa simu) bila ruhusa wala mkataba
Wanamuziki wa kongwe wa Bongo Flava AY na Mwana FA wamezawadiwa kulipwa kiasi cha Sh.2.18 billioni za kitanzania baada ya kwenda kuwashtaki mtandao wa TIGO kwa kutumia nyimbo zao pasipo makubaliano yao.
Mahakama ilitoa amri hiyo kuashiri kua TIGO ilikutwa na hatia ya kuharibu hati miliki za nyimbo za wasanii hao kwa kuziuza kama miito ya simu bila kukubaliano nao kimkataba.
Mkuu wa wilaya mstaafu Bw. Juma Hassan alikubaliana na utoaji wa pesa hizo April 11,2016 baada ya mlolongo na ufuatiliaji uliyochukua miaka minne wa kesi hii. Pia kiasi kingine cha Sh millioni 25 kiliongezwa kwa ajili ya usumbufu na uharibifu wa jumla kwa wasanii hao.
Habari hizi zimekuja kusikika maskioni mwa watu kuanzia Jumanne hii baada ya kesi kupelekwa mahakama kuu baada ya kua ikikawia kutafutiwa suluhisho.
Mwana FA alisema kua huu ni muda wa mabadiliko baada ya wasanii wengi wa nyuma kukumbwa na matatizo kama haya na hati zao miliki kutumiwa vibaya .
Baada ya mahojianiano na Mwanamuziki AY alisema pia kua “Hiki ni kitu ambacho kimekua kikitokea mara nyingi na kwa muda mrefu sana na yote ni kwa sababu ya kukosa uelewa na pia uhitaji wa pesa kuendesha kesi kama hizi” pia
AY aliongezea na kusema kwamba “Hakuna mtu anaruhusiwa kutumia kazi ya msanii yeyote bila ruhusa ya muhusika au makubaliano na kama kunafaida iliyopatikana bhasi muhiska wa hiyo kazi apewe kulingana na thamani ya kazi yake”
Mwana FA na Ay waliomba kulipwa kaisi cha biliioni za kitanzani Sh4.3 wakidai kua TIGO walipata hela nyingi sana kupitia miito yao amabyo ilitamba hadi nje ya nchi.
Post by :Eye De Marie
Post a Comment