0

Kwa Mujibu wa Mtandao wa millardayo Umeripoti  taarifa kuhusu waimbaji wa muziki wa bongofleva Alikiba na Baraka Da Prince ambao wote wako chini ya lebo ya Rockstar 4000, kuvamiwa na Majambazi wenye silaha Afrika Kusini saa tatu usiku kwa saa za Afrika Mashariki July 20 2016.

1_ Management inayowasimamia Imeuambia mtandao wa millardayo  kwamba wawili hawa pamoja na watu wengine wakati wanavamiwa, walikua kwenye eneo kulikofanyika kikao cha maandalizi ya kazi zilizowapeleka Afrika Kusini kwa siku saba.

2_Majambazi hao walikua sita na walikua pia na silaha za moto (bunduki)

3_Miongoni mwa vitu walivyoibiwa ni pamoja na simu zao za mkononi ambapo Majambazi hao wakati wote wa tukio waliwanyooshea Bunduki kina Alikiba kuwatisha zaidi na bila kutaka kupoteza muda.

4_Baraka Da Prince na Alikiba wote ni wazima wa afya na hawakurudhika na chochote kwenye hilo tukio

5_Pamoja na tukio hili kutokea, Baraka na Alikiba hawatosimama kufanya projects zao… wamechukua mapumziko mafupi na kisha wataendelea.
Credit To Millard

Post a Comment

 
Top