Msanii kutoka Tanzania, Diamond Platnumz ameipa tena heshima kubwa bendera ya nchi yake kwa kuingia kwenye kipengele cha msanii bora wa Kimataifa (Best International Act).

Hii ni hatua kubwa kwa Diamond baada ya siku chache tu nyuma kutangazwa kuingia kwenye tuz
o za MTV Base (Mama Awards).
bet1 Diamond Platnumz kwenye kipengele hiki cha tuzo kubwa za televisheni ya burudani BET ya Marekani, yupo kama Best International Act Africa na anawania tuzo hii na wasanii kama Davido kutoka Nigeria, Mafikizolo kutoka Afrika Kusini, Tiwa Savage kutoka Nigeria, Toofan na Sarkodie wa Ghana. BET imetumia twitter kutoa hii taarifa kuthibitisha tiki kwa Diamond na kuumpa hongera kama msanii pekee kutoka Afrika Mashariki. Hongera mwana, Diamond Platnumz!!
ASANTE KWAKUTEMBELEA WEBSITE HII JIUNGE NASI KUWA MWANA FAMILIA WA JIMMCARTER.COM FACEBOOK-JIMCARTERTZ | TWITTER JIMMCARTERTZ
Post a Comment