Kundi la Navy Kenzo linaloundwa na producer na muimbaji Nahreel pamoja na girlfriend wake Aika wako nchini Afrika Kusini, walikoenda kutumbuiza kwenye tamasha la African Music Concert (AMC 2015).
Baada ya tamasha hilo lililofanyika Jumamosi Nov. 21 jijini Johannesburg, na kuwakutanisha wasanii mbalimbali wa Afrika kwenye jukwaa moja kama Davido, Wizkid, Vanessa Mdee, Victoria Kimani na wengine, hit makers wa ‘Game’, Navy Kenzo walipata fursa ya kuingia studio kurekodi collabo na kundi la R2Bees kutoka nchini Ghana.
“Something z comin @navykenzoofficial ft @r2beesmusic #goodmusiconly” aliandika Nahreel Instagram.
R2Bees ni kundi linaloundwa na wasanii wawili ambao ni ndugu (binamu), Faisal Hakeem (Paedae da Pralem) na Rashid Mugeez (Mugeez).
Miongoni mwa tuzo kubwa walizowahi kushindania ni pamoja na BET Awards 2013 ‘Best International Act: Africa’, na ni washindi wa tuzo 9 za Ghana Music Awards.
WAFAHAMU HAPA KWENYE HII VIDEO

Post a Comment