0

Katibu mkuu kiongozi Ombeni Sefue amepiga marufuku utengenezaji na uchapishaji wa kadi za Krismass na mwaka mpya kwa gharama za Serikali mwaka huu.

Balozi Sefue ameelekeza kuwa yeyote anayetaka kutengeneza ama kuchapisha kazdi hizo afanye kwa gharama zake mwenyewe.

Taarifa hito iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi wa mawasiliano Gerson Msigwa imesema fedha zilizopangwa kugharamia utengenezaji wa uchapishaji wa kadi hizo utumike kupunguza madeni ambayo Wizara, idara na Taasis za umma zinadaiwa na wananchi waliotoa huduma na bidhaa kwao au zipelekwe katika matumizi mengine.

Taarifa hiyo ilisomeka kama hivi

Post a Comment

 
Top