0

Ninaamini utakuwa umeshausikia wimbo mpya wa Judith Wambura aka Lady Jaydee ‘NASIMAMA’ ambao video yake iliyoongozwa na Hefemi pamoja na audio yake iliyofanywa Sharobaro Records vimetoka hivi karibuni na kupokelewa vizuri.  Kwa mujibu wa Tovuti ya Times FM, mtunzi wa wimbo huo ni msanii mpya aitwaye Barakah Da Prince ambaye pia ametambulisha single yake mpya ‘JICHUNGE’ takribani mwezi mmoja uliopita.

 Hii inathibitisha kwamba pamoja na ukongwe na mafanikio makubwa aliyoishayapata Jide lakini bado anapenda kushirikisha mawazo ya watu wengine katika kazi zake bila kujali umaarufu wa mtu. Tovuti hiyo ilizungumza exclusive na Barakah Da Prince ili kufahamu yeye kama mtunzi wa ‘Nasimama’ amehusika kwa kiasi gani. “Aah wimbo wa ‘Nasimama’, nakumbuka kipindi hicho bado nilikuwa kwa Bob Junior pale, ilikuwa ni mwaka jana ,na Bob Junior aliniita mimi kipindi hicho, akanipigia simu akaniambia Barakah njoo studio kuna kazi inabidi tufanye hapa kazi ya Jide[...] nimefika pale akaniambia Lady Jaydee leo anakuja usiku kurekodi wimbo na inabidi tumuandalie nyimbo yeye atakuja turekodi. “ Alisema Barakah.“Nikamwambia poa basi bahati mbaya umeme kwa wakati huo ulikuwa umekatika ukaweza kurudi usiku, kwahiyo usiku ndo akaniambia nimtafutie chords tukawa tunajaribu kupiga chords flani hivi nzuri zikawa zinakataa, nikamwambia kwanini tusipige chords ambayo inaweza kwendana na wimbo wa Yahaya?”.



 Akaendelea, “Nikawa naimba imba akaniambia basi tutafute kitu kinachoweza kwendana na chords zile, nikatafuta chorus ambayo ndo ‘aliyepanga ni manani, shida na riziki zangu’, nikawa naimba hivyo nikampa na chords kabisa nikawa namwimbia chords inabidi zipigwe hivi , akapiga chords za beat na kick na vitu vingine vingine.”“Kwahiyo ule wimbo nimehusika kuanzia idea ni ya kwangu, melody ni ya kwangu, hata pia idea ya beat ilikuwa yangu na hata uandishi wa nyimbo nzima ni mimi ingawa katika uandishi tulisaidiana na kijana mmoja anaitwa Man More ni msanii wa pale kwa Bob Junior kwenye verse ya kwanza tu lakini, ndio tumesaidiana na Man More na Man More kaandika mistari kama mitatu minne [...] hiyo nyimbo ina verse mbili[...] verse ya pili na chorus ni mimi mwenyewe, verse ya kwanza tumesaidizana na Man More lakini melody za verse zote ni za kwangu ni mashahiri tu tumesaidizana kidogo.” Alisema Barakah Da Prince kutoka Mwanza. 


“Jide alikuwepo sababu Jide alifika muda huo na Gadner, na alipofika muda ule alikuta tayari beat imeshagongwa mpaka chorus imepatikana kwahiyo tulikuwa tunaandika verse. Na nakumbuka huo wimbo kabla ya verse ya kwanza tuliandika kwanza verse ya pili hiyo ndio ilikuwa inatakiwa iwe verse ya kwanza, sema tukashauriana hiyo verse ya pili nzima nzima nimeandika mimi, Bob Junior akasema hii haitapendeza sana ikikaa verse ya kwanza itapendeza ikikaa verse ya pili, ndio tukaandika verse nyingine na hiyo verse nyingine wakati tunaiandika alikuwepo Lady Jaydee, Gadner, mimi na Man More.” Barakah aliendelea kueleza, “Ni nyimbo nyingi sana ambazo nimeandika sio kwamba ni hii tu ya Lady Jaydee, kuna nyimbo nyingi ambazo zinatokea Sharobaro ambazo nimeandika, na sio kwamba navyokuwa nafanya waga eti nataka credit kwamba mimi ndio nimeandika wimbo flani hapana waga siko hivyo, sema mtu mwenyewe kama akipenda mwenyewe kutoa credit ni yeye, asiipopenda pia lakini lakini mi waga naandika kumsaidia mtu.Tulikuwa tunasaidizana tu kama mi ambavyo naweza nikahitaji msaada wake Jide akanisaidia kama msanii mwenzake.” Alipoulizwa kama amewahi kumtafuta Bob Junior au Lady Jaydee toka wimbo huo umetoka: “Sikuweza kumtafuta mtu yeyote sijamtafuta Bob Junior wala sijawasiliana na Jide wala mtu yeyote sijaongea naye, kutokana mi na Bob kuna mtafaruku ambao ulikuwepo mdogo sana kipindi cha nyuma enzi zile nilikuwa chini ya Bob Junior , na kutokana kuna vitu ambavyo vilifanya mimi nikaweza kutoka Sharobaro hadi nikafika Tetemesha, kwahiyo sikutaka kuwauliza mi nimeshangaa tu wimbo unatoka na video inatoka.”
 Barakah aliongeza kuwa katika verse ya pili ukiusikiliza vizuri ‘Nasimama’ kuna sehemu ambayo sauti ya kiume inamwitikia Jaydee, kwenye dakika ya 2:31 kwenye maneno haya “Moyo wa mtu kichakaa, mengi yaliyofichika, unayemdhania mwema, kumbe mchawi kwako”. hiyo sauti inayoitikia hapo ni ya Barakah. Gadner G.Habash ambaye ni meneja wa Lady Jaydee alizungumza pia na Tovuti hiyo iliyotaka uthibitisho kama wasanii hao wawili wa Sharobaro ndio watunzi wa wimbo huo. “Kuna vijana wawili ambao walihusika, lakini mmoja ambaye ndiye aliingiza sauti kwenye verse ya pili kama ukisikiliza vizuri kuna sauti ya kiume kwenye verse ya pili sehemu fulani[...] huyo ndiye alihusika kwa kiasi kikubwa sana japo simkumbuki jina.” Alisema Gardner. “Muulize tu kama ndiye aliyeingiza sauti basi ndiye huyo aliyefanya sehemu kubwa sana ya wimbo.” Bob Junior ambaye ndiye producer wa ‘NASIMAMA’ kupitia studio yake ya Sharobaro Records alizungumzia uwezo wa wasanii wake waliohusika kuuandika wimbo wa Jide. Kuhusu Barakah ambaye alikuwa akifanya kazi kabla hajaenda Tetemesha aliuelezea uwezo wake alisema :“Ni mwanamuziki mzuri, anajua, anajua kuandika anajua kuimba anajua yaani, ni msanii mzuri, ni msanii ambaye unaweza kumuita msanii.”

JIUNGE NASI  KUWA MWANA FAMILIA WA JIMMCARTER.COM

Post a Comment

 
Top