0

Studio Ya Mwanalizombe inayomilikiwa na legend wa muziki wa Hip Hop Joseph Haule a.k.a Profesa Jay haina muda mrefu toka ianzishwe lakini tayari imeshaanza kutoa kazi zinazofanya vizuri ikiwemo single mpya ya D-Knob aliyomshirikisha Mwasiti ‘Nishike mkono’ iliyofanywa na producer Villy.Profesa Jay amesema Mwanalizombe Studio haitakuwa Inafanya Audio peke yake, hivi karibuni wanatarajia kuanza kufanya videos pia.

“video tumeagiza vyombo kwasababu kuna vitu ambavyo tunavyo lakini kuna lights ambazo hatuwezi kufanya kazi bila zenyewe”, Amefunguka Profesa Jay kupitia kipindi cha Sunrise cha Times FM leo.“So tumeagiza tunategemea soon or later kila kitu kitakuwa kimekamilika tutaanza kushoot video. Tunafanya vitu vingi pale ndio maana inaitwa Mwanalizombe studios, hatukutaka tuandike Mwanalizombe Records kwasababu ingekuwa ni audio tu peke yake.” Amesema Jay Jay ambaye hivi sasa ana single mpya ‘Kipi sijasikia’ ameongeza kuwa tayari Mwanalizombe imeanza kupata wasanii kutoka nje ya Tanzania ikiwa ni pamoja na Kenya na Sudan ya Kusini wanaokuja kurekodi.

Jiunge Nasi hapa Chini  Kuwa Mwana  Familia  Wa Jimmcarter.com

                               FOLLOW  US ON FACEBOOK  FOR MORE UP DATES CLICK HERE

Post a Comment

 
Top