Baada ya Ben Pol kudai kuwa hatoweka tena nyimbo zake kwenye biashara ya ringtone,hit maker wa ‘Roho Yangu’ Rich Mavoko amesema ameshindwa kuingiza wimbo wake wa Roho Yangu kwenye mfumo wa ringtone kwa kudai kuwa wasanii wanavyonywa na haoni umuhimu wake. Akizungumza na tovuti ya Times FM, Rich amesema hajawahi kupata faida yoyote. “Nyimbo zangu nyingi za mwanzo zimekuwa kwenye ringtone na sijapata faida yeyote kwenye ringtone. I swear to God sijapata faida yoyote kwenye ringtone za kibongo wala sioni umuhimu wa ringtone kama tunavyonyonywa wasanii.
Mimi nitakuwa msanii wa kwanza wakisema tunatoa hiyo system…kwa sababu sipati faida yoyote zaidi ya kupata stress. Yaani kumfuata mtu kuanza kumwambia malipo yangu…mimi nimeimba halafu wewe unisumbue mimi. Na unapokuja na makaratasi yako kusaini unaniomba mwanangu utapata asilimia hizi, sipati asilimia zozote. Roho Yangu siwezi kuiuza huko, inabidi niuze nyimbo kama nyimbo,” alisema.
Jiunge Nasi hapa Chini Kuwa Mwana Familia Wa Jimmcarter.com
Post a Comment