Klabu ya Azam FC imeanza rasmi
maandalizi ya kutetea ubingwa wao msimu ujao na michuano ya kimataifa kwa
kukamilisha usajili wa mchezaji wa kimataifa wa Burundi aliyekuwa anakipiga
kwenye klabu ya Yanga.
Taarifa rasmi zilizothibitishwa na
meneja wa Azam FC Jemedari Said ni kwamba mshambuliaji Didier Kavumbagu
amejiunga na klabu hiyo kwa mkataba wa mwaka mmoja.“Ni kweli Kavumbagu tumemalizana nae
na amesaini mkataba wa mwaka mmoja.
Taarifa zaidi zitatolewa baadae.” Alikaririwa Jemedari.Kavumbagu alitua nchini Tanzania akitokea Burundi alipokuwa anaitumikia Vital O na kuja kujiunga na Yanga misimu miwili iliyopita
ASANTE KWAKUTEMBELEA WEBSITE HII JIUNGE NASI KUWA MWANA FAMILIA WA JIMMCARTER.COM
Post a Comment