0

 Kocha wa zamani wa Barcelona, Tito Vilanova aliyekua akipambana na ugonjwa wa saratani(cancer) kwa miaka michache iliyopita hatimaye jana jioni amefariki dunia. Vilanova alifanyiwa upasuaji siku ya Alhamisi lakini upasuaji huo haukuweza kuokoa maisha yake na gonjwa hilo kuchukua maisha yake hapo jana. FC Barcelona ikiwa na matatizo ya uwanjani wiki za karibuni,jana imeingiwa na machungu mapya zaidi baada ya kocha wake wa zamani, Tito Vilanova kufariki dunia kwa ugonjwa wa saratani akiwa na miaka 45.


 Klabu ya FC Barcelona katika akaunti yake ya twitter ilisema: “FC Barcelona ipo katika huzuni. Tito Vilanova amefariki akiwa na umri wa miaka 45. Apumzike kwa amani,”. Vilanova aliteuliwa kuwa kocha wa Barcelona mwishoni mwa msimu wa 2011-12 na akawawezesha Barcelona kusawazisha rekodi ya Real Madrid kumaliza msimu na pointi 100. Alianza kuwa Msaidizi wa Pep Guardiola mwaka 2008.

Jiunge Nasi hapa Chini  Kuwa Mwana  Familia  Wa Jimmcarter.com

                                        FOLLOW  US ON FACEBOOK  FOR MORE UP DATES CLICK HERE

Post a Comment

 
Top