0

Dr. Dre yupo njiani kuwa rapper wa kwanza BILLIONAIRE pale kampuni ya Apple itakapoinunua kampuni yake yake Beats Electronics.  Dre  Kwa mujibu wa TMZ, Apple inadaiwa itainunua Beats kwa gharama ya $3.2 BILLION.

Dre na mwanzilishi wa Interscope, Jimmy Iovine ndio walioanzisha kampuni hiyo.
 Dre na Jimmy walianzisha kampuni hiyo mwaka 2008 kwa kutengeneza headphone lakini sasa wanatengeneza pia spika, vifaa vya sauti vya kwenye magari na mtandao wa kustream muziki.
 Deal hiyo inaweza kukamilika wiki ijayo na itakuwa deal kubwa zaidi ya kampuni Apple. Dre alikamata nafasi ya pili kwenye orodha ya Forbes ya wasanii wa hip hop matajiri zaidi akiwa na $550 million nyuma ya Diddy mwenye $700 million.

ASANTE KWAKUTEMBELEA WEBSITE  HII JIUNGE NASI  KUWA MWANA FAMILIA WA JIMMCARTER.COM FACEBOOK-JIMCARTERTZ | TWITTER JIMMCARTERTZ

Post a Comment

 
Top