Wakati mashabiki wa klabu ya Newcastle Utd wakiendelea kutoa shinikizo kwa mmiliki wa klabu hiyo Mike Ashley, ili afanye maamuzi ya kumtimua mkuu wa benchi la ufundi Alan Scott Pardew, hali imeendelea kuwa tete kwa meneja huyo kutoka nchini Uingereza.
Tangu mwanzoni mwa msimu huu Newcastle Utd wamekua na matokeo mabovu tofauti na ilivyokuwa inatarajiwa, hali ambayo imeendelea kuongeza hasira kwa mashabiki ambao wanahitaji kuiona The Magpies ikisogea kutoka ilipo sasa na kupiga hatua.
Alan Pardew, amekiri wazi kwamba ana hali ngumu klabuni hapo na anaamini matokeo yanayoendelea kumuandama hayatomsaidia chochote katika harakati za kulinda kibarua chake zaidi ya kusaka ushindi kuanzia mchezo ujao.
Amesema ni vigumu kuwaridhisha watu wote kwa wakati mmoja, lakini hana budi kufanya kazi yake ipasavyo kwani alipewa jukumu la kuwa meneja wa Newcastle Utd kwa ajili ya kusaka mafanikio nasi karaha kwa mashabiki:: Credit Times Fm
ASANTE KWAKUTEMBELEA WEBSITE HII JIUNGE NASI KUWA MWANA FAMILIA WA JIMMCARTER.COM FACEBOOK-JIMCARTERTZ | TWITTER JIMMCARTERTZ INSTAGRAM JIMCARTERTZ

Post a Comment