Bishoo, Quick Rocka amekanusha kuwa na Uhusiano wa kimapenzi na muigizaji wa filamu, Kajala Masanja
Akizungumza na 255 ya XXL, Clouds FM, Quick amesema ana girlfriend hivyo uvumi huo unaweza ukamharibia uhusiano wake.
“Nasema hapana Kajala mimi sister yangu, tunafanya naye kazi na nimeunganishwa na Lamata.
Lamata ni director ninayemmfahamu zamani kidogo kipindi kile tunafanya ‘Mbwa Mwitu’ tulikuwa wote, Lamatah, Hemedy! Unajua mnavyofanya movie ni tofauti na kufanya video, kwa mfano wakati tunafanya ile movie ya Wolper, tulikaa Magomeni kambini ili kujenga chemistry.
Unajua mnapoigiza kuna vitu lazima viendane. Sisi ni kambi moja inabidi mchongo tuufanikishe,” Alisema Quick Rocka.
“I have a girlfriend, anavyosikia hivi vitu mimi kwa upande mmoja inaniharibia na sijui yeye pia ana mtu wake huko kwahiyo tuna wazazi, tuna watu wetu wa karibu ambao wanatuangalia, watu ambao wametupenda na wametuamini hivyo halafu wakija kusikia mambo haya kwenye media wataona kumbe huwa hamfanyi kazi, wao wanachukulia serious. Sio vitu vya kweli.”
JIMMCARTER.COM WANAKUTAKIA HERI YA SIKUKU NA MAANDALIZI MEMA YA SIKUKU YA CHRISTMAS NA MWAKA MPYA PIA TUNAKUKRIBISHA KUJIUNGA NASI HAPA CHINI




Post a Comment