Baada ya kuhusishwa kwenye drama ya Chris Brown na Karrueche Tran weekend iliyopita, sasa inadaiwa kuwa rapper wa Canada, Drake amelazwa hospitali baada ya kujihusisha kwenye ugomvi na P.Diddy.
Mtandao wa Page Six umeripoti kuwa rapper Drake amegombana na kushikana mashati na Puff Daddy nje ya club flani huko Miami jumatatu asubuhi ya November 24.
Pia Kwa mujibu wa TMZ, Diddy alimfunza adabu Drake nje ya club ya Miami Jumatatu asubuhi ambapo wote walikuwa wamehudhuria birthday ya Dj Khalid.
Mwanzo ilisemekana kuwa sababu ilikuwa ni mpenzi wa Diddy aitwaye Cassie, lakini chanzo kingine kiliuambia mtandao huo kuwa sababu ilikuwa ni mambo ya biashara.
Shuhuda mmoja amedai kuwa wakati wa ugomvi huo inasemekana Diddy alisikika akimwambia Drake “kamwe huwezi kunikosea heshima” na kisha kumshushia konde moja.
JIMMCARTER.COM WANAKUTAKIA HERI YA SIKUKU NA MAANDALIZI MEMA YA SIKUKU YA CHRISTMAS NA MWAKA MPYA PIA TUNAKUKRIBISHA KUJIUNGA NASI HAPA CHINI




Post a Comment