0

Album mpya ya J.Cole, 2014 Forest Hills Drive imeuza kopi nyingi zaidi kwenye wiki ya kwanza kuliko album yoyote ya hip hop iliyotoka mwaka huu.

Rekodi hiyo ilikuwa ikishikiliwa na album ya Rick Ross, Mastermind iliyouza kopi 179,000 kwenye wiki yake ya kwanza. Album ya Cole imeizidi mara mbili Mastermind kwa kuuza kopi 361,000 kwenye wiki ya kwanza. 

Pamoja na hivyo, 2014 Forest Hills Drive imevunja rekodi kwa kusikilizwa mara milioni 15.7 kwenye wiki yake ya kwanza na kuvunja rekodi ya kundi la One Direction iliyosikilizwa mara milioni 11.5. 014 Forest Hills Drive imeuza zaidi kwenye wiki ya kwanza tangu album ya Eminem, Marshall Mathers LP 2 ya mwaka jana iliyouza kopi 792,000 kwenye wiki ya kwanza. Album hiyo imetoka bila kuwa na single redioni.

Post a Comment

 
Top