0

Watu wengi wanafahamu wimbo wa Aiyola pekee wa Harmonize kuwa ndio umetengenezwa kwenye studio za Wasafi Records zinazomilikiwa na msanii Diamond baada ya kuamua kumsamimia msanii huyo.

Lakini Diamond kupitia ukarasa wake wa facebook ameweka wazi kazi nyingine za muziki zilzofanyika kwenye studio hizo ikiwemo audio ya tangazo la voda la Ongea Deilee ambalo limeimbwa msanii huyo pia wimbo wa Sweet Love wa Akothee toka kenya ambao pia msanii huyo ameshirikishwa.

“Kama Hauna taarifa bado Tangazo hili la VODACOM ONGEA DEILEE la Audio limefanyika kwenye studio yetu ya #‎WasafiRecords‬ chini ya Producer wetu LAIZER…Nyimbo ya @Akotheekenya ‪#‎SweeLove‬ pia inetengezwa #WasafiRecords ,Albam yangu Mpya, Ngoma Mpya na Albam ya @harmonize_tz , Na Ujio Mpya wa @raymondtiptop pia zote zimepikwa toka #WasafiRecords… soon zitakuwa Masikioni Mwako!!!!!!!!!!!!!!! @wcb_wasafi for Life!!✊” amepost Diamond
kwenye ukarasa wake wa instagram“

Post a Comment

 
Top