Diamond akiwa amevaa nguo ya
Roperrope ambayo designer wake mmarekani alidai kuwa ni feki
Devontae Roper, ni designer wa Los
Angeles, California, Marekani ambaye ametokea kujipatia umaarufu kwa nguo zake
zinazovaliwa na mastaa wa muziki nchini humo wakiwemo August Alsina, YG, Chris
Brown, Future na wengine. Brand yake inajulikana kwa jina la RoperRope.
Devontae Roper
Juzi Roper alipost picha ya Diamond
Platnumz akiwa amevaa nguo zenye mfanano na designs zake na kumchana staa huyo
kuwa ameiba ubunifu wake kupitia yule Diamond aliyemuita kama ‘designer’ wake
ambaye kazi yake hasa ni ‘stylist’.
“I usually don’t blast people who
make or wear fakes of my designs but this person went way too far when they
used my logo! @diamondplatnumz is wearing fake #Roperrope shirt made by a
person with bad character and a strong lack or originality! This is not ok! If
you steal a design please reframe from using the Designers Logo because it’s
illegal www.shoproperrope.com,” aliandika kwenye Instagram.
Post hiyo ambayo hata hivyo tayari
imefutwa ilisababisha mjadala mkubwa na wengi iliwafanya wamfahamu Roper ambaye
nguo zake zimekuwa zikionekana kwenye video nyingi za August Alsina, Future na
Chris Brown.
Wapo waliomshutumu Diamond na kudai
kuwa ameumbuka lakini wengi walimtetea na kwa kusema yeye ni mvaaji tu wa nguo
hizo na hana kosa hata kama alivaa nguo feki.
Mimi ni mmoja watu niliokuwa na
mtazamo tofauti. Hii nipost niliyoweika Instagram kutoa ushauri wangu:
“Hili suala mimi nalionea katika
muktadha chanya zaidi. Designer anayewavalisha August Alsina, Future, Meek
Mill, Draya na wengine kamlalamikia Diamond kuvaa nguo feki zinazoiga brand
yake. Naamini Diamond hana kosa kama lipo labda ni kumuita ‘stylist’ wake
‘designer’ na hivyo kuhisi Diamond anavaa nguo zake feki zilizotengenezwa na
designer wa Diamond ambaye basically kazi yake ni kumchagulia bosi wake nguo za
kuvaa. Binafsi mimi leo ndo nimemjua roperrope na nina uhakika wengi pia
wamemjua leo thanks to Diamond. That means roper kapata exposure kubwa Tanzania
na zaidi ya hapo. Diamond na roper wanaweza kufanya kitu pamoja. Hakuna shaka
kuwa Diamond ni fan wa design zake na anaweza kumudu gharama za kupata
customised outfits kutoka kwake na huenda akawa brand ambassador wake Mkubwa
Afrika. Wanasema everything happens for a reason and I think this is not just a
coincidence but something that was planned by a higher force (God).
@diamondplatnumz make the most of this encounter and I bet you gonna be one of
the best dressed African entertainers.”
Roper aliweka post ya pili Inayo onekana hapo juu kusisitiza
kile alichokisema awali na kudai kuwa hakumuuzia Diamond nguo hizo. Hapo ndipo
watu wengi waliifahamu vyema drama hiyo kiasi cha kuanza kuhisi kuwa designer
huyo anatafuta umaarufu.
Roper alipost picha nyingine ya
Diamond na kuandika: Bless Up emoji🏼 I just got news #Roperrope just went International emoji God
is everywhere #YoungGod x #ICantLose #ShippingOverseas #ThanksEastAfrica
#GodFlow @DiamondPlatnumz hit me up next time.”
Post a Comment