Rapa Jay Moe alikuwa kwenye #FridayNiteLive ya EATV na kufunguka kuhusu kurudi kwenye game la rap lenye ushindani mkubwa sana kwa sasa pakiwa na majina kama Fid Q, Joh Makini, Bilnass na Nikki Wa Pili.
Jay Moe anasema hajarudi kwenye game la muziki ili kushindana na wasanii wanaofanya vizuri, bali amerudi ili kukata kiu ya muziki kwa mashabiki wake ambao walikuwa wanamsubiria kwa muda mrefu.
Jay Moe “Mimi sijarudi kwenye game ili nishindane na waliopo, nimekuja kutoa burudani kwa mashabiki wangu ambao walinimis kwa muda mrefu, pia nikikutana na hao wasanii ambao mnawasema wananiambia Jay Moe bado game linakuhitaji, kwa hiyo mimi narudi kwenye game ili kutoa burudani kwa mashabiki wetu, kwa sababu mimi naamini mashabiki wa Joh Makini na wasanii wengine ndio wale wale mashabiki wa Jay Moe,”
Jay Moe ametoa video mpya inaitwa ‘Pesa Ya Madafu’.
Post a Comment