![]() |
Samatta katika picha ya pamoja na Wazriri Nape, Waziri Lukuvi na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi (kulia). |
Samatta katika picha ya pamoja na Wazriri Nape, Waziri Lukuvi na Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi (kulia).
![]() |
Kutoka kulia ni Waziri Lukuvi, Mbwana Samatta na Waziri wa Habari, Vijana, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye. |
IKIWA ni kuthamini tuzo aliyotwaa nahodha wa timu taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta ya Mchezaji Bora wa Soka Afrika kwa wachezaji wa ndani, Serikali kupitia wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, jana imemzawadia nyota huyo kiwanja cha kujenga makazi kilichopo eneo la Kigamboni jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kujali na kuthamini heshima ambayo Samatta ameiletea Tanzania ya kuwa mwanasoka bora wa Afrika kwa wachezaji wanaocheza ndani (ligi za Afrika).
Samatta amepewa kiwanja na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Lukuvi kwenye sherehe maalum ya kumpongeza Mbwana Samatta kwa kutwaa tuzo hiyo iliyoipa heshima kubwa Tanzania, jana usiku Hyatt jijini Dar es Salaam.
Mbwana Samatta aliishukuru serikali kwa kutambua mchango wake katika soka la ndani, sapoti ya serikali katika masuala ya soka na michezo kwa ujumla huku akiiomba serikali kuweka mikakati endelevu ya kuendeleza soka nakuibua vipaji zaidi ili wapatikane akina Samatta wengi zaidi.
Kwa upande mwingine, Samatta aliwashukuru Watanzania na wadau wote wa michezo wanaomuunga mkono. Samatta amesema amekuwa akifarijika tokea arejee nyumbani na tuzo ya Mwanasoka Bora Afrika anayecheza Afrika kutokana na Watanzania kuendelea kumfariji.
“Naendelea kusema tena ninashukuru kwa sapoti yenu, najua nimesema hivi mara kadhaa. Lakini si vibaya kushukuru tena” alisema.
Samatta amezidi kuwa gumzo na lulu baada ya kufanikiwa kutwaa tuzo hiyo ya mwanasoka bora Afrika na kuweka rekodi mpya Tanzania.
Post a Comment