Wiki kadhaa zilizopita ilisambaa hii clip ambayo ilikuwa ikimuonyesha rapa Dudu Baya akimtukana matusi mazito msanii wa Bongo Flava Shetta.
Katika video hiyo Dudu alitukana matusi mazito ya nguoni huku akimtishia kumpiga.
Sasa leo kupitia ukurasa wake wa Instagram, mkali huyu aliyevuma zamani ameamua kuandika waraka wa kumuomba msamaha Shetta huku akidai kuwa alizidiwa na ulevi wa kupindukia.
“Habari zenu mashabiki zangu? Ningependa kuchukua nafasi hii leo maalumu kwa ajili ya kumuomba samahani mdogo wangu NURDIN BILAL @officialshetta kwa ajili maneno machafu na matusi niliyowahi kukutukana kwenye kipande cha video kilichosambaa sana kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo facebook,instagram,youtube n.k. So ningependa kuchukua nafasi hii adhimu kuweza kukuomba msamaha kwa lile jambo lilitokea kwani kusema ukweli kabisa sikuwa kwenye hali yangu ya kawaida kwani nilikuwa nimelewa sana pombe. So mimi kama kaka yako GODFREY TUMAINI a.k.a DUDUBAYA naomba tuweze kusamehena makosa yote tuliyoyafanya mimi na wewe kwa kupishana kauli au kutoolewana kwa jambo lolote lile. Kwani binafsi yangu mimi kama mimi nimekusamehe kabisa kwa moyo mmoja kama kuna kosa lolote lile uliloniwahi kunifanyia na ningependa na wewe mdogo wangu uweze kunisamehe kwa jambo lolote lile nililowahi kukukosea mdogo wangu. Kwani sisi wote ni binadamu na tumeumbwa kukosea na kusamehena. So naomba sana tuweze kusamehana na tuweze kuangalia zaidi mziki wetu, maisha yetu na familia zetu kwa ujumla @officialshetta @officialshetta” Ameandika Dudu Baya
Post a Comment