0

Mama kijacho Blac Chyna ameweka picha ya “ultra sound” ya mwanae mtarajiwa  katika account yake ya Instagram na kuandika ujumbe huu akikumbushia jinsi ambavyo alikua akidhania furaha yake imekamilika kabla ya kukutana na mchumba wake Rob Kardashian

Blac Chyna aliweka picha na kuweka “caption” ya ujumbe huu; 

“ Kwa muda mrefu nilihisi kua King angekua mwanangu wa pekee. Na kwamba yeye angekua baraka yangu kubwa na tungeishi kwa furaha milele tukiwa mimi na yeye tu,

nilikua sitafuti mtu wa kua nae kimapenzi kwasababu nilihisi nina kila kitu nachokihitaji.Lakini angalia Mungu alivyo wa ajabu! Leo nimeposwa na kutarajia kuolewa na moja kati ya wanaume ambao ananipenda mimi pamoja na King huku tukitarajia furaha nyingine!

 Nataka kusema kua usikate tamaa na uwe na matumaini kwasababu hata yadhaniwayo kua ni hadithi hutimia”

Post a Comment

 
Top