0
Msanii wa Kimataifa kutoka nchini Marekani Neyo aliwasili jijini Mwanza jana  jioni akitokea Dar es Salaam na kupokelewa na umati mkubwa wa wakazi wa jiji hilo kama Mfalme katika Uwanja wa Ndege wa jijini Mwanza.

Msanii huyo anatarajiwa kutumbuiza katika tamasha la Jembeka Festival 2016  kwa kupiga ‘Live Music’ katika uwanja wa CCM Kirumba ambapo wasanii wa kimataifa kutoka nchini, Diamond Platnumz, FID Q, Stamina, Mr. Blue, Ney wa Mitego, Maua Sama, Rubby, Baraka Da Prince, Juma Nature, MO Music na wengine wengi watapanda jukwaa moja na msanii Neyo.

Balozi wa Umoja wa Mataifa mtoto mwanabadiliko wa mazingira, Getrude Clement akimvisha shuka la kimasai Msanii wa Kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo baada ya kuwasili jijini Mwanza leo jioni.

Mwanasheria wa Jembe Media Group, Justine Ndege katika picha ya pamoja na Msanii wa kimataifa kutoka nchini Marekani, Neyo katika hoteli ya Malaika Resort.


Post a Comment

 
Top