Rapper Iggy anadai kuwa ex wake alikopi data nyingi kutoka kwenye laptop yake bila ruhusa.
Iggy amefungua mashtaka hayo dhidi ya Hefe Wine kwa kumtuhumu kudownload kila kitu kutoka kwenye komputa yake binafsi mwaka 2009 wakati wakiishi pamoja huko Atlanta.
Anadai kuwa data hizo ni pamoja na nyimbo ambazo hakuwahi kuzitoa.
Iggy anamtuhumu pia ex wake huyo kwa kufoji nyaraka alizodai kuwa alisaini mkataba ambao utamruhusu kusambaza nyimbo na video zake.
Hata hivyo mashtaka hayo hayajataja chochote kuhusu mkanda wa ngono ambao Hefe anadai kuwa walirekodi.


Post a Comment