![]() |
| Javier Hernandez anaweza kutimkia Real Madrid. |
Unaweza kusikia kuhama kwa mshambuliaji wa Manchester United Javier Hernandez kwenda Real Madrid.
Queens Park Rangers wanahusishwa na kuhama kwa mshambuliaji wa zamani wa Spurs Jermain Defoe. Klabu ya Toronto FC ya Canada imeeleza kuwa itakuwa na furaha zaidi kurejea kwa mshambuliaji huyo wa zamani wa Uingereza.
West Ham United nao wamegeuza kibao kwa mlinzi wa Manchester City Micah Richards.
Richards, 26, anajiandaa kujiunga Fiorentina kwa mkopo. Mshahara wake utakuwa pauni 75,000 kwa wiki, Micah ameonekana kuwa tatizo kwa Hammers.
Baada ya West Ham kugoma kumnyakuwa Fiorentina wameonyesha nia na Micah Richards. Lakini sasa tunasikia kwamba mchezaji Nick Powell wa Man U anatarajiwa kuhamia Leicester kwa mkopo.
Baada ya tetesi kwamba mshambuliaji Radamel Falcao atajiunga na Real Madrid kugonga mwamba, inaonekana kwamba Manchester City ndio wako mbioni kumnyakuwa.
![]() |
| Real Madrid. Hapana. Radamel Falcao anaweza kuondoka Monaco na kwenda Etihad. |
Hata hivyo Alvaro Negredo amefunguliwa mlango na kwenda Valencia, na kutoa nafasi City kwa ajili ya kumleta mshambuliaji wa kati. Arturo Vidal na Danny Welbeck nao pia wanaweza kuondoka kwenye vilabu vyao.




Post a Comment