Rapper amuua mkewe na kujiua, mkewe alimsaliti na Trey Songz, Mayweather ashuhudia tukio zima la mauaji!
Hayes alikuwa ameumizwa na uhusiano wa kimapenzi aliokuwa nao mke wake na Trey Songz. Stephanie Moseley aliuawa nyumbani kwao na mume wake huyo huko Los Angeles.
![]() |
| Rapper Hayes |
Vyanzo vilivyo karibu Hayes, vimeuambia mtandao wa TMZ kuwa Hayes alitengana na mke wake miaka miwili iliyopita baada ya kugundua alimsaliti na Songz.
Walirudiana lakini Hayes hakuwa amepona kidonda cha kusalitiwa na kwenye mazungumzo yao mara nyingi alikuwa akikumbushia suala la Songz.Trey ametweet:R.I.P babygirl. Once an angel on earth, now watching over us from Heaven. You’ll b missed but never forgotten.
![]() |
| Chris Brown na Stephanie |
Hayes na Moseley walifunga ndoa mwaka 2008 na marafiki zao wanasema alikuwa akimpenda mno mke wake. Chanzo kingine kimeuambia mtandao wa HollywoodLife.com kuwa Hayes alikuwa anaendelea kumhisi mke wake anamsaliti kabla ya kumuua.
![]() |
| TREY |
Kimesema Stephanie alikuwa anataka kumuacha mumewe kutokana na tabia
yake ya kumchunga muda wote. Kimeongeza kuwa rapper huyo aliwahi
kutishia kujiua kama mke wake angemuacha na kweli Stephanie alikuwa
amuache miezi miwili iliyopita.
Katika hatua nyingine, mtandao wa TMZ umedai kuwa bondia Floyd
Mayweather alikuwa akiwasiliana na Hayes aliyekuwa rafiki yake kupitia
mtandao wa video wa FaceTime na alishuhudia yote yaliyotokea.
Rapper huyo alimpigia Floyd kutumia FaceTime Jumatatu asubuhi akiwa
amekasirika kutokana na madai kuwa mke wake si mwaminifu. Kwa mujibu wa
vyanzo, Earl alisema angemuua mke wake. Bondia huyo alijitahidi kumuomba
asichukue uamuzi huo lakini alishindwa.
Floyd hajasema alichoona lakini amekubali kuwa alikuwa shuhuda na
alisikia kila kitu. Floyd yupo kwenye wakati mgumu kutokana na tukio
hilo.
JIMMCARTER.COM WANAKUTAKIA HERI YA SIKUKU NA MAANDALIZI MEMA YA SIKUKU YA CHRISTMAS NA MWAKA MPYA PIA TUNAKUKRIBISHA KUJIUNGA NASI HAPA CHINI








Post a Comment