Roma anatarajia kuachia single mpya Ijumaa hii iitwayo ‘Mwanakondoo’, ikiwa ni zawadi kwa mashabiki wake katika siku yake ya kuzaliwa Dec.12.
“Kesho ni birthday yangu (Dec.12), kwahiyo nikaona katika zile stock za ngoma za Roma tuchukue moja wapo iwe kama zawadi hivi kwa mashabiki wangu, sijawahi kufanya chochote kile kwenye birthday yangu.” Amesema Roma .
Roma pia ameelezea maana ya wimbo huo: “Mwanakondoo ni wimbo flani ambao umekaa ki-Mungu kabisa, kiupako kabisa.
Tafsiri ya mwanakondoo kwanini tumeita kondoo kwasababu kondoo ni mnyama mpole, msikivu, mtaratibu, kwahiyo mwanakondoo kwa sisi wakristo tunaamini Yesu Kristo ni kondoo wa Mungu, na sisi hapa ni wanakondoo kwamba tunahitaji mchungaji ili twende.
Kwahiyo mimi ni muumini ambaye nasali naomba Mungu sema nakuwa sifanikiwi katika kile nachokisali, inafikia muda nakataa tamaa nahisi labda Mungu hayupo ndio maana hanisikilizi.
Katika huo wimbo kuna sauti ya Stamina, kwahiyo Stamina anakuja na kuniplease kwamba Mungu yupo amini katika sala, maombi ipo siku utafanikiwa, kwahiyo ni wimbo flani wa kuwahamasisha watu wazidi kupiga goti kumwomba Mungu.”
JIMMCARTER.COM WANAKUTAKIA HERI YA SIKUKU NA MAANDALIZI MEMA YA SIKUKU YA CHRISTMAS NA MWAKA MPYA PIA TUNAKUKRIBISHA KUJIUNGA NASI HAPA CHINI



Post a Comment