0



Tulizowea kuonaVuta N’kuvute kwenye klabu za mpira wakishindana kusajili wachezaji nakupandisha dau kubwa sasa imehamia vituo vya redio na inaendelea na sasa East Africa Radio imekuwa mhanga mpya.

Mrembo Dj wa kike, Sinyorita na mtangazaji wa The Cruise, Mami wanadaiwa kuondoka East Africa Radio kuanzia wiki hii baada ya kupata dau kubwa kutoka kwa guess what? Clouds FM.
Tetesi hizo zilianza kuvuma tangu wiki iliyopita lakini jana zimeonekana kupata ukweli baada ya wawili hao kutosikika kwenye kipindi cha The Cruise, kitu ambacho si cha kawaida.
Tetesi zinadai kuwa tangu Dj Fetty aache kazi Clouds FM, wamekuwa wakitafuta mtangazaji wa kike anayeweza kuchukua nafasi yake na Mami anaonesha kuwa na caliber hiyo.

Tayari wawili hao wamebadilisha profile zao za Instagram kwa kuondoa kipengele cha kuwa ni wafanyakazi wa East Africa Radio.
sasa zinasomeka hivii
Wawili hao wanatarajiwa kutambulishwa rasmi kwenye kituo chao kipya cha kazi soon.
Nini maoni yako kuhusu hili tasnia ya habari inakuwa na ushindani kwa tanzania kwa sasa?

Post a Comment

 
Top