0
Kama wewe ni namba moja fan wa Mtangazaji wa BBC Swahili  Mtanzania Salim Kikeke basi utakuwa umemmiss kwa muda flani hivi amelitambua hili na amewakumbuka nakuandika ujumbe huu hapa chini kupitia ukurasawake wa facebook.

"Asanteni sana kwa salaam zenu. Bado niko kwenye likizo ya uzazi. Naomba radhi kwa wasanii wachanga kwa kushindwa kurusha kazi zenu kwa muda sasa kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wangu, hali kadhalika kwa mashabiki wa habari mbalimbali za ulimwengu pamoja na za michezo kumekuwa kimya kidogo lakini msiwe na shaka tutaendelea hivi karibuni. 
Nichukue nafasi hii pia kuwatambulisha kwa bwana mdogo Ioan (Yoan) Issa Kikeke. 
Kwa mapenzi yake Mola nitarejea kazini mwisho wa mwezi huu wa Aprili. Shukran sana na Mwenyezi Mungu awabariki sana." Ameandika Salim Kikeke



Post a Comment

 
Top