Kamati ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge imewatia hatiani wabunge saba kwa makosa mbalimbali ikiwemo kudharau madaraka ya bunge. Wabunge Easther Bulaya na Tundu Lissu wameadhibiwa kutokuhudhuria vikao vilivyobaki vya mkutano wa tatu na vikao vyote vya mkutano wa nne.
Wabunge Pauline Geku, Halima Mdee, Zitto Kabwe, Godbless Lema wasiudhurie vikao vyote vilivyobaki vya mkutano wa tatu na Mbunge John Heche hatahudhuria vikao kumi vya mkutano wa tatu. Makosa hayo waliyafanya mkutano wa pili mwezi January.
Jumla ya wabunge 7 wamesimamishwa kuhudhuria vikao vya bunge kwa kosa la kusimama bila kufuata utaratibu
Wabunge Bulaya na Lissu wameadhibiwa kutohudhuria vikao vilivyobaki vya mkutano wa tatu na vikao vyote vya mkutano wa nne
Wabunge Pauline Gekul, Halima Mdee, Zitto Kabwe, Godbless Lema wameadhibiwa kutokuhudhuria vikao vyote vilivyobaki vya mkutano wa 3
Mbunge John Heche hatohudhuria vikao kumi vya mkutano wa tatu
Maneno ya Zitto baada ya kufungiwa kwa utovu wa Nidhamu kwa kamati ya maadili


Post a Comment