Ngoma ya Drake “One Dance” inayofanya vizuri Kwa wiki ya pili katika nafasi ya kwanza ya “Billboard 100 Hot” imeonekana kumganda na kua tiba ya mwanamuziki Justin Bieber.
Hit maker huyo wa “Sorry”, Justin Bieber ameamua kuweka wazi kuipenda nyimbo hiyo na kuamua kufanya Remix.
Kwa mara ya kwanza Remix hiyo ilisikika katika kipande cha video kilichopostiwa na muigizaji maarufu Marekani Gabrielle Union katika akaunti yake ya SnapChat. Muigizaji huyo alikua akijirusha katika club moja ya Monaco weekend hii na kuiskia nyimbo hiyo ikirushwa hewani na Dj.
Katika clip hiyo yakasikika haya maneno “Mimi sijui jina lako, lakini nina uhakika wewe wanijua ” ikiwa ni sehemu ya nyimbo hiyo iliyofika mpaka Twitter. Bado haijawekewa uhakika kama hiyo Remix ni rasmi au ni Justin Bieber Mwenyewe kaamua tu kuimba.
Dj pia alisikika akisema “ Hii ni mara ya kwanza mtu kuisikia” wakati akiachilia nyimbo hiyo hewani kwa mara ya kwanza katika club hiyo.
Ngoma hiyo ya Drake inafanya vizuri sana katika chati mbali mbali ikiwa kama “Number 1 hit song”.
Unaweza ukaisikiliza hiyo Remix kwa mara ya kwanza kwa kubonyeza play.
Justin x drake remix!!! Ahh pic.twitter.com/UYNNWwtM0m— jb (@Jelysandra) May 29, 2016
Part 2 of the another snippet lol pic.twitter.com/LSpUnPw8iW— jb (@Jelysandra) May 29, 2016

Post a Comment