Kutoka kwenye dili la viatu la Puma mpaka kwenye dili la miwani la Manolo Blahnik, Rihanna amechukua sekta nzima ya mitindo dunini kwa kasi sana. Na sasa mkali huyu wa mitindo amepata dili kubwa la mitindo na kampuni kubwa ya miwani ijulikanayo kama “Dior”.
Kama sehemu ya bidhaa zake na ubalozi, muimbaji huyu anaetamba na kibao chake cha “work” kwa sasa anashirikiana na mwanamitindo wa kifaransa katika utengenezaji wa style ya miwani ambayo imepewa jina kama “RIHANNA”. Kwa mujibu wa WWD (Women’s Wear Daily) frames za mawani hayo zitaanza uzwa tofauti kwa reja reja kuanzia mwezi huu wa sita.
Mtindo huu mpya wa mawani unapatikana katika rangi za silver,nyekundu,kijani, blue na pink. Zitauwa kwa bei ya reja reja ya $840, na kama zikiwekwa kipande cha dhahabu pembezoni bhasi itakua na gharama ya $1,950.
Hii si mara ya kwanza Riri kufanya kazi na Dior. Mwaka jana, mwanamuziki huyu mwenye miaka 28 alitajwa na kampuni hiyo ya Dior kama mwanamke wa kwanza mweusi kua msemaji mkuu katika kampeni yao ya "Secret Garden IV" iliyofanywa na Steven Klein katika mji wa Versailles huko Ufaransa.
“Tunafurahi sana kwa kushirikiana kwa mara nyingine na Rihanna” alisema Afisa mtendaji mkuu wa Dior mwenye jina la Sydney Toledano, Pia aliendelea na kusema kua “yeye ni msanii, mburudishaji, mwekezaji na ni mwanamitindo anaetazamwa na wengi katika kizazi cha leo”
Rihanna alitembelea makao makuu ya Dior mwezi wa kumi kwa ajili ya ubunifu wa mawani hayo.Ubunifu wa miwani hiyo wa 2000 ulitokana na lutein kamanda Geordi La Forge kutoka kwenye movie ya “Star Trek”.
Rihanna alisema, “ Nimekua daima nikipenda uvaaji wake wa miwani, na nilipofika katika kampuni ya Dior na kuona vifaa vyote ambavyo nilikua naweza kucheza navyo kubuni kitu, mawazo yangu yote yalikamilika hapo”
Wakati ukiwa bado kwa ajili ya kuitangaza miwani hiyo, mpiga picha Jean-Baptise Mondino alimpiga picha mwanadada Rihanna kwa ajili ya kuandaa bidhaa hizo endelezi kwa matangazo rasmi.
Rihanna pia akiwa kama ni mkurugenzi mbunifu wa style ya sandals za puma, hivi karibuni alizindua bidhaa zake za viatu ambayo imepewa jina kama “Denim Desserts” akishirikiana na Manolo Blahnik na kufunga dili hilo kwa millioni $10 na LVMH Moet Hennessy Lous Vuitton ambayo pia ni kampui inayojulikana huko Ufaransa..






Post a Comment