JB akanusha kugombana na Steve Nyerere kwa deal la matangazo Muigizaji wa filamu, Jacob Stephen aka JB amekanusha tetesi
za kupigana na mwenyekiti wake Steve Nyerere kutokana madai ya kuzungukana
katika deal la matangazo.
JB
JB, amedai kuwa hawezi kufanya kitu kama hicho kwani Steve
Nyerere ni mwenyekiti wake. “Jamani mimi nimeshawaambia mimi ni mtu mzima jamani, Steve
Nyerere ni mwenyekiti na ni mtu ambaye ninamuheshimu, hakuna kitu kama hicho
mbwa acheni mambo yenu, mimi ni mtu mzima na familia, kwahiyo mambo kama haya
siwezi fanya, kwenye msiba mimi sijagombana chairman wangu, nashangaa watu
wanalikuza hili suala.
STIVE
Jamani Steve Nyenyere ni kiongozi wangu,” alisema JB kwa
hasira. Mtandao wa bongo movies pamoja na mingine imedai kuwa baada
ya mazishi ya muigizaji na muongozaji wongozaji wa filamu marehemu Adam Philip
Kuambiana, JB na Steve Nyerere wanadaiwa walishikana na kupigana kutokana na
kuzungukana katika mambo ya matangazo
Post a Comment