0
The Game Aonyesha Upendo Wa Ajabu Kwa Prince Kwa Kutumia Miilioni 150 Za Kibongo Kwa kupamba  sebule yake. 

Mwanamuziki The Game ameamua kupambisha sebule yake kwa “purple rain” (mvua ya zambalau” kwa kutengeneza picha yenye sura ya marehemu Prince Rogers Nelson kwa rangi ya zambarau ikiashiria “purple rain” ikiwa ni moja katika jina la nyimbo za marehemu Prince…Shukrani kwa uchoraji huo ikiwa ni kwa heshima ya marehemu Prince

Vyanzo zinasema The Game alimuajiri mchoraji aitwaye “Madstreets” siku ambayo Prince alifariki dunia na kumuomba amtengenezee mchoro huo kwa heshima ya Prince. Rappa The game alikua  bado kidogo afanye ngoma na marehemu  kabla hajafariki. 
Tunaambiwa The game alitumia kiasi cha USD 65000  kwa ajili ya mchoro huo, ambapo ilimchukua mchoraji Madstreets masaa 100 kumaliza kazi hiyo. Picha hiyo inaukubwa wa ‘8x6’ ni rangi za mafuta, akriliki na dawa za rangi mbali mbali zilitumika kupambisha picha hiyo na jumapili picha hiyo iliweza kuwekwa sebuleni kwa The Game kama ionekanavyo kwenye picha.

Post a Comment

 
Top