Ziara ya Kilimanjaro Music Tour ambayo ndio gumzo kubwa sasa katika
sekta ya
burudani imebisha hodi katika Mji wa Moshi ambapo wapenzi wa muziki
wanatarajiwa
kupata burudani ya aina yake kutoka kwa wasanii mbalimbali Jumamosi
hii.
Maandalizi yote yamekamilika huku zaidi ya wasanii 10 wa humu nchini
wakitarajiwa
kutua mjini hapo Ijumaa tayari kwa show kubwa itakayofanyika katika
Viwanja vya Chuo
Shirikishi cha Ushirika na Biashara (MUCCOBs).
Ziara hii inadhaminiwa na Bia ya Kilimanajro Premium Lager ambayo
imekuwa mstari
wa mbele katika kufikisha muziki wa Tanzania kwenye kilele cha
mafanikio. Ziara hii
inaratibiwa na EATV na East Africa Radio, Executive Solutions,
Integrated na AIM.
Wasanii watakaotoa burudani ni pamoja na Ommy Dimpoz, Kala Jeremiah,
Weusi, Ben
Pol, Jambo Squad, Young Killer, Ney wa Mitego, Mwana FA, Khadija Kopa,
Warriors na
Professor J.
“Wasanii wote wako tayari kutoa burudani ya aina yake na sisi kama
wadhamini
tunawaahidi wakazi wa Moshi mambo mazuri...waje kwa wingi wakutane na
wasanii
wao na pia wapate burudani bila kusahau Bia yao namba moja Kilimanjaro
Premium
Lager,” alisema Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George
Kavishe.
Alisema kiingilio katika show hii itakayoanza saa nne asubuhi ni Tsh
2500 na kila
atakayeingia atapewa bia ya bure mradi ametimiza umri wa miaka 18 na
show itaanza
saa nne asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni.
Tiketi wa ajili ya show hii zitaanza kuuzwa siku ya Ijumaa pale MUCCOBs
na pia
promosheni mbalimbali za kusisimua zinaendelea katika baa tofauti Mjini
Moshi.
“Ziara hii sio ya washindi wa Tuzo za Muziki (Kilimanjaro Music Awards)
bali ni ziara ya
wasanii ili waweze kutangaza kazi zao pamoja na kupeleka burudani
mikoani ili watu
wanaokaa huko pia waweze kufaidi,” alisema Bw Kavishe.
Aliongeza kuwa wasanii wana nafasi kubwa sana kueneza ujumbe mbalimbali
katika
jamii hivyo wanapaswa kuungwa mkono ili waweze kuwafikia wananchi
wakiwemo wa
mikoani.
Ziara hii itahusisha mikoa ya Moshi, Mwanza, Kigoma, Kahama, Iringa,
Mbeya,
Dodoma, Tanga, Mtwara na Dar es Salaam na inaanzia Mkoani Moshi Mei 24,
Mwanza
Mei 31, Kahama Juni 7, Kigoma Juni 14, Iringa Juni 21, Mbeya Agosti 9,
Dodoma
Agosti 16, Tanga Agosti 23, Mtwara Agosti 30, Dar es Salaam Septemba
6,” alisema
Kavishe.
ASANTE KWAKUTEMBELEA WEBSITE HII JIUNGE NASI KUWA MWANA FAMILIA WA JIMMCARTER.COM FACEBOOK-JIMCARTERTZ | TWITTER JIMMCARTERTZ
Post a Comment