Rihanna ameimwaga label yake ya muda mrefu Ya Def Jam
Records na kujiunga na label inayoongozwa na Shawn Carter aka Jay Z, Roc
Nation, Kwa mujibu wa jarida la Complex lilivyomeripoti.
Pamoja na Ririhana (26) kuachana na Def Jam lakini album yake
ijayo ambayo itakuwa inafuata baada ya ‘Unapologetic’ ya mwaka 2012, itaendelea
kusambazwa na label hiyo.

Awali Jay Z ndiye aliyemsaini Rihanna kipindi alipokuwa bado
ni rais wa Def Jam kabla hajajiondoa mwaka 2009 na kuanzisha Roc Nation, lakini
uhusiano wao wa kikazi uliendelea kama kawaida.
ASANTE KWAKUTEMBELEA WEBSITE HII JIUNGE NASI KUWA MWANA FAMILIA WA JIMMCARTER.COM
Post a Comment