Song: mguu pande
mguu sawa Artist: stamina
ft walter chilambo Studio: one love
fx Producer; tiddy
hotter Song writer: stamina
(verse),walter (choruss)Intro;staminaYeaaah,,,u know what tiddy One love fx again men Iz moro town in da house Shorwebwenzi on this one Vers 1(stamina)Peleka kitanda batani,kama unapenda ukeshe bar/ Sista duu muda hausimami,hata uivulie nguo saa/ Ishi kiushujaa,kama umepanga kambi ya jeshi/ Kati ya maarufu na star,maarufu anaongoza kwa deshi/ Ewe raisi wa wanyama,fanya sensa usisahau/ Mfuasi aliyesaliti chama,huku mjini bonge la nyau/ Tunza bible sio irizi,ufalme wa mbingu hauna fensi/ Ndo maana akifaga mzinzi,mazishi hatufanyi gesti/ Chagua kilicho best,kati ya copy na kupaste/ Je Yule aliyefeli maisha na class alifeli test?/ Hakuna demu anayejiuza,hicho ndo nikijuacho/ Nachojua wanakodisha,unatumia huondoki nacho/ Bitozi msaka mchumba,usiforce unapotemwa/ Piga goti kwa muumba,ikibidi akuumbe tena/ Mguu mmoja pande,mwingine urudishe sawa/ Hiyo ndo ishara ya kiafande,ya kuweka mambo sawa/ Chorus(walter chilambo)Naamini kama nyuma ulikosea rudi Weka mambo sawa na plan b Unaweza fanya bora zaidi (muda bado) Mguu pande(mojaaaaa)mguu sawa(mojaaaaa) Nyuma geuka(moja mbili tatu mojaaa)…..x2 Mguu pandeeee(mojaaaaaa)mguu sawa(mojaaaa) Nyuma geukaaaaaa. Vers 2(stamina)Mjini wanyama kibao,cha ajabu wanakula unga/ Mawazo ya vichwa vyao,dingi afe warithi nyumba/ Ewe kengeza,chunga usimcheke chongo/ Cha msingi muombe ebeneza,akupe vision yenye michongo/ Saka chaka kila sehemu,maana pesa ina machale/ Nyie mnaowinda mademu,hivi mna nyota ya mshale?/ Mnyamazie mshenzi,ukimjibu tu anatuna/ Hadi shoga nae ana mpenzi?,kweli madem mna huruma/ Mziki umejaa stress,ambazo haziishagi kwa pombe/ Mastar wamewekeza desi,wanakufa hawana hata ng’ombe/ Underground chondechonde,usiache shule kisa mziki/ Usuperstar una mabonde,na miteremko ya dhiki/ Yesu anarudi lini?,hilo swali ndo ujiulize/ Sio stamina utaoa lini,nitajibu tu niko bize/ Mguu mmoja pande,mwingine urudishe sawa/ Hiyo ndo ishara ya kiafande,ya kuweka mambo sawa/ Chorus(walter chilambo)Naamini kama nyuma ulikosea rudi Weka mambo sawa na plan b Unaweza fanya bora zaidi (muda bado) Mguu pande(mojaaaaa)mguu sawa(mojaaaaa) Nyuma geuka(moja mbili tatu mojaaa)…..x2 Mguu pandeeee(mojaaaaaa)mguu sawa(mojaaaa) Nyuma geukaaaaaa. Vers 3(stamina)Usitupe mayai kiholela,zalisha ili uache chata/ Maisha baiskeli ya delela,ukiinama chako unapata/ Kumpa kibogoyo mnofu,kisa nyama bei aghali/ Ni sawa na kumteta kipofu,huku kifikra anaona mbali/ Hakuna zali la mentali,kwenye sayari ya kupendwa/ Mlevi mnywa safari,je unajua unapokwenda?/ Acha mashauzi,sista duu genge linalipa/ Ujanja sio kwenda south,au china ili ukawe striper/ Mapenzi ni kutendwa,mpendaji jiamini/ Sharo ukiona unapendwa,ujue una nyota ya ukimwi/ Ni sawa na uote,usiku una kiss na jini/ Halafu uamke ujikute,una lips stick kwenye ulimi/ Unahitaji akili,sio mashavu yenye dimpoz/ Mwanaume jasiri,hajichubui kisa ana pimpoz/ Mguu mmoja pande,mwingine urudishe sawa/ Hiyo ndo ishara ya kiafande,ya kuweka mambo sawa/ Chorus(walter chilambo)Naamini kama nyuma ulikosea rudi Weka mambo sawa na plan b Unaweza fanya bora zaidi (muda bado) Mguu pande(mojaaaaa)mguu sawa(mojaaaaa) Nyuma geuka(moja mbili tatu mojaaa)…..x2 Mguu pandeeee(mojaaaaaa)mguu sawa(mojaaaa) Nyuma geukaaaaaa.
Post a Comment