Diamond Platnumz ndiye msanii namba moja kwa sasa nchini Tanzania baada ya usiku wa Jumamosi kunyakua vipengele vyote zote saba alivyokuwa ametajwa kwenye tuzo za muziki za Kilimanjaro, KTMA.

Muimbaji huyo aliyekuwa ameambatana na mchumba wake Wema Sepetu amechukua tuzo ya wimbo bora wa mwaka, wimbo bora wa afro pop na video bora ya mwaka kwa wimbo wake ‘My Number On’e pamoja na Muimbaji Bora wa kiume – Kizazi Kipya, Mtumbuizaji bora wa kiume wa muziki na Mtunzi Bora wa Mwaka – Kizazi Kipya.
Meneja wa bia ya Kilimanjaro, George Kavishe (kulia) akimkabidhi tuzo Diamond, kushoto ni producer wa My Number One, Sheddy Clever Wema akimkumbatia Diamond
Msanii mwingine aliyeshangaliwa zaidi katika usiku wa tuzo hizo ni Fid Q aliyenyakua tuzo mbili ambazo ni Msanii Bora wa Hip Hop na Mtunzi Bora wa Mwaka – Hip Hop.

Na kundi la Weusi limeibuka na tuzo mbili, Wimbo bora wa Hip Hop (Nje ya Box – Nick wa Pili ft Joh Makini & G-Nako) na Kikundi cha mwaka cha kizazi kipya.

Chini hapo Vanessa Mdee akimbusu Lulu baada ya kukabidhiwa tuzo ya wimbo bora wa R&B

Mzee wa badilisha Jose Chameleone akipokea tuzo ya wimbo bora wa Afrika Mashariki
Isha Ramadhan akipokea tuzo Wasanii waliotumbuiza
Wasanii wa Kenya, Amani na Wyre wakimkabidhi tuzo Luiza Mbutu
Usiku Wa ulipambwa na wasanii Mwana FA, Weusi, Madee, Vanessa Mdee, Meninah, Angel, Makomando, Msami, Twanga Pepeta, Extra Bongo na wengine.
Orodha nzima Ya Washindi Wa Zuzo hUsiku wa kill. Wimbo bora wa mwaka Number One – Diamond
Mwimbaji bora wa kike – kizazi kipya Lady Jaydee M
uimbaji Bora wa kiume – Kizazi Kipya Diamond
Muimbaji bora wa kike taarab Isha Ramadhan
Muimbaji Bora wa kiume – Taarab Mzee Yusuf
Muimbaji bora wa kiume – Bendi Jose Mara
Muimbaji Bora wa Kike – bendi Luiza Mbutu
Msanii Bora wa Hip Hop Fid Q
Msanii Bora Chipukizi Anayechipukia Young Killer
Rapa Bora wa Mwaka – Bendi Furguson
Mtumbuizaji bora wa kike muziki Isha Ramadhani
Mtumbuizaji bora wa kiume wa muziki Diamond
Mtunzi Bora wa Mwaka – Hip Hop Fid Q
Video Bora ya Mwaka Number One – Diamond
Bendi ya Mwaka Mashujaa Band
Kikundi cha Mwaka cha Taarab Jahazi Modern Taarab
Kikundi cha mwaka cha kizazi kipya Weusi
Mtayarishaji bora wa nyimbo wa mwaka – Taarab Enrico
Mtayarishaji bora wa nyimbo wa mwaka – Kizazi kipya Man Walter
Mtayarishaji bora wa nyimbo wa mwaka – Bendi Amoroso
Mtunzi Bora wa Mwaka – Taarab Mzee Yusuf
Mtunzi Bora wa Mwaka – Kizazi Kipya Diamond
Mtunzi Bora wa Mwaka – Bendi Christian Bella
Wimbo bora wa Kiswahili – Bendi Ushamba Mzigo – Mashujaa Band
Wimbo bora wa reggae Niwe na Wewe – Dabo
Wimbo bora wa Afrika Mashariki Tubonge – Jose Chameleone
Wimbo bora wa Afro Pop Number One – Diamond
Wimbo bora wa Taarab Wasiwasi Wako – Mzee Yusuf
Wimbo bora wa Hip Hop Nje ya Box – Nick wa Pili f/ Joh Makini & G-Nako
Wimbo Bora wa R&B Closer – Vanessa Mdee
Wimbo Bora wa Kushirikiana Muziki Gani – Nay wa Mitego ft Diamond
Wimbo bora wa ragga/dancehall Nishai – Chibwa f/ Juru
Wimbo bora wa zouk /rhumba Yahaya – Lady Jaydee
Hall of FAME Award Hassan Rehani Bichuka
Masoud Masoud – TBC Taifa
ASANTE KWAKUTEMBELEA WEBSITE HII JIUNGE NASI KUWA MWANA FAMILIA WA JIMMCARTER.COM
Post a Comment