Baba mdogo, Mama mdogo wa rapper Stereo pamoja na ndugu zake wengine wanne waliofariki usiku wa kumikia Jumamosi kutokana na ajali ya moto, wanatarajiwa kuzikwa Jumanne hii katika makaburi ya Air wing Ukonga Banana jijini Dar es Salaam.
Akizungumza kwa uchungu kwenye 255 ya XXL kupitia Clouds FM, Stereo alisema hawataweza kutoa heshima za mwisho kwa miili ya marehemu hao kutokana kuungua sana kiasi cha kutotambulika.
“Waliofariki dunia ni watu sita,kuna baba yangu mdogo ambaye yeye ni last born wa marehemu baba yangu ni baba mmoja mama mmoja, mke wake baba mdogo, mjomba wangu ambaye ni ndugu wa mwisho wa marehemu mama mdogo, brother ambaye ni mtoto wa mzee pia kulikuwa na watoto wawili wa brother wangu wa mwisho ambaye yupo na yeye yupo kwa sababu hakuwepo nyumbani wakati wa tukio,” alisema Stereo.
“Kwa mujibu wa vyanzo vilivyonipatia habari ni kwamba moto huo unasemekana ni wa shoti ya umeme, sasa hatujui moja kwa moja hiyo shoti ilianzia sehemu gani? Lakini watu wanasema moto ulikuwa mkubwa sana na nguvu ya watu ilikuwa ndogo ukilinganisha na ukubwa wa janga lenyewe,” aliongea Stereo.
“Moto ulikuwa mkali sana ngumu hata kusogea then walijaribu kuwapigia simu zima moto lakini zimamoto hawakuweza kufika eneo la tukio mapema walichelewa sana walifika saa moja asubuhi wakati tukio likiwa limetokea saa nane usiku.
Sasa unaweza ukapata picha kama kuna mtu alikuwa anaungua tangu saa nane usiku hadi saa kumi na mbili asubuhi huwezi kukuta kitu.
Miili imeungua sana yaani wameungua sana kiasi kwamba hatuwezi hata kuwaaga na hatutaweza kuwafunua kwa sababu wameungua sana.”
Credit To:: Bongofive
Post a Comment