0


Msanii wa muziki kutoka Kenya mwenye asili ya Kiburundi, Kidum anazikamata headlines za leo baada ya taarifa kusambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa msanii huyo mwenye hit single ya Namba Moja amemgeukia Mungu kuwa mwokozi wa maisha yake!
Nimekutana na stori kwenye mtandao wa The Citizen inayosema siku ya jumatatu wiki hii Mchungaji ajulikanae kwa jina la Eric Omba alichukuwa time na kushara na watu wake kupitia page yake ya Instagram picha zake akiwa anambatiza msanii huyo na kuandika caption ya maneno inayosema…
“Baada ya kuokoka, Kidum sasa ameamua kusimama kwenye uwokovu kwa kumgeukia Yesu Kristo. Nina furaha kubwa sana kama mchungaji aliyepata fursa ya kumbatiza upya kaka yangu. Amekiri mbele ya dunia nzima kuwa Yesu Krisoto ni mwokozi wa maisha yake.” nukuu kutoka mtandao wa The Citizen.

Kidum ameshafanya kazi kadhaa za Gospel ikiwa pamoja na kuachia nyimbo kama Mungu Anaweza na Kimbia ila sasa amerudi upya kumtumikia Mungu kwa levo ya juu zaidi.

Ukiacha mbali kazi zake za Gospel, Kidum pia alifanikiwa kutoa hit singles kadhaa kama Haturudi Nyuma ngoma alioshirikisha Juliana msanii kutoka Uganda na Nitafanya single aliohirikisha mkongwe wa R&B Tanzania, Lady Jay Dee.
Historia ya Kidum kwenye kurasa za burudani ilianza mwaka 1995 alipoenda Kenya kunusuru maisha yake kutokana na hali ya kisiasa iliyokuwa inaendelea Burundi na toka kipindi hicho Kidum aliweza kujitengenezea jina kama msanii wa muziki Kenya, ambapo alipata pia fursa ya kusafiri nchi mbalimbali kutangaza muziki wake.

Post a Comment

 
Top