Rapper Mwana FA amesema wasanii kuipokea vizuri ‘Asanteni Kwa Kuja‘ ni heshima kubwa sana, anafikiria kufanya collabo ikiwezekana zitatokea zaidi ya moja au mbili huku mastaa kama Fid Q, Jay Moe na Solo Thang wakiwa kwenye mstari mzuri kutia sauti kwenye mdundo huo.
Kinachoendelea mpaka sasa ni mipango tu ambayo Mbunge Joseph Haule ‘Prof. Jay‘ na mrembo yoyote kati ya Vee Money na Maua Sama nao huenda wakawepo kwenye remix ya ‘Asanteni kwa Kuja’ !!
Kama umeona washkaji wa Mapacha wako kimya hivi kwenye muziki wana mipango mingine 2016, wamesema wanakuja na show ya TV ambayo itahusu maisha yao zaidi… show imepewa jina la 50/50 show, vikwazo ni vingi so jamaa imebidi wajikusanye mkwanja kwa muda mrefu ili mzigo ukamilike na kwenda hewani.
Naomba nikusogezee updates kuhusu mipango ya collabo ya Mb Dog kufanya collabo na Lil Wayne, Manager Q S Mhonda amesema mipango ipo na itakamilika mwaka huuhuu 2016 huku Chris Brown akiingia ya kwenye list ya collabo na Mb Dog…
kingine sasahivi wanafatilia mchongo wa kuhakikisha jamaa hao wawili wanatua TZ kwa ajili ya kupiga show na kufanya collabo au Mb Dog kusafiri kwenda Marekani kukamilisha mzigo.
BONYEZA PLAY KUSIKILIZA SAUTI
BONYEZA PLAY KUSIKILIZA SAUTI
Post a Comment