Wakati mashabiki wa Jay Z wakitegemea kusikia chochote kutoka kwa Rapper huyo, Memphis bleek, rafiki wa karibu wa Jay Z anaamini mmiliki huyo wa Roc Nation anaweza asiachie tena album.
Akifanya mahojiano na The Breakfast Club, Memphis bleek alisema kwasasa Jay Z anaweza akaachia baadhi ya nyimbo tu lakini anadhani ni ngumu kwa rapper huyo kutulia studio na kuaandaa album nzima.
“I don’t know if he’s retired,” Alisema Memphis “but I don’t know if he’ll ever drop another album.” Aliongeza “might drop songs here and there,” it’s unlikely Jay would block out the time necessary to craft a proper solo LP: “Imagine what it would take to get Jay in the studio to lay a verse.”
Hata hivyo hivi karibuni kulikua na tetesi za kuwa Jay Z alikua anaandaa album ya pamoja na Beyonce.
Album ya mwisho ya Jay Z ilikuwa Magna Carta Holy Grail iliyotoka mwaka 2013.
TAZAMA VIDEO YA MAHOJIANO HAPA!!
Post a Comment