0

RIP: Watanzania wamlilia Edwin Semzaba, mwandishi wa kitabu cha Ngoswe Mwandishi wa vitabu vya Kiswahili kikiwemo, Ngoswe: Penzi Kitovu cha Uzembe, Edwin Semzaba amefariki dunia Jumapili ya January, 17. 

Alikuwa mhadhiri wa chuo kikuu cha Dar es Salaam, UDSM kwenye idara ya sanaa za maonesho. Semzaba anakumbukwa kwa uandishi wake mahiri hususan kwa kitabu cha mchezo wa Ngoswe; Penzi Kitovu cha Uzembe kilichotumika kwenye shule za sekondari katika somo la Kiswahili. 
Marehemu Edwin Semzaba, kulia
 Baadhi ya vitabu vya hadithi alivyoandika ni pamoja na Marimba ya Majaliwa, 2008, Funke Bugebuge, 1999, Tausi wa Alfajiri, 1996 na Tamaa ya Boimandaa, 2002 Michezo aliyoiandika ni pamoja na Kinyamkera, 2014, Joseph na Josephine, , 2014, Mkokoteni, 2014, Tendehogo na Sofia wa Gongolambotoa 1985. Semzaba amewahi kushinda tuzo nyingi za uandishi wa vitabu. 

 Hivi ndivyo watu walivyotuma salamu zao za rambirambi.




Post a Comment

 
Top