0

Producer Scott Storch wa Marekani hakupenda kuona Mtanzania Lamar kapost beat yake Instagram? tazama comments zake

Jana February 23 2016 Producer Mtanzania Lamar alipost video akiwa studio kwake na spika zikitoa mdundo mmoja mkali alafu akaandika caption yenye swali, watu wacomment kumwambia 

Msanii gani atafaa kupita juu ya huo mdundo kisha akamtag producer Scott Storch kwamba ndio anampa Inspiration, yani kazi ya Scott inamvutia na anajifunza vingi kutoka kwake.
A video posted by Agent DAF (@lamarfishcrab) on



Scott Storch Akiwa Na Tyga
Inabidi ufahamu kwamba Scott Storch (42 yrs) ni producer maarufu wa Marekani ambaye mikono yake ilihusika kuzitengeneza beats za hits nyingi ikiwemo Naughty Girl ya Beyonce, Sorry ya Rick Ross na Chris Brown, pia Make It Rain ya Fat Joe na Lil Wayne.

Sasa comment ya kwanza ya Scott baada ya kuona hii post ya Lamar ni swali, 





@scottstorchofficia lWhy do u have my beat on your ig
Kwanini unaweka beat zangu kwenye Instagram yako?

Lamar akamjibu…
lamarfishcrab @scottstorchofficial Welcome to your world boss.. I'm a huge fan! Keep inspiring us.

 Karibu kwenye ulimwengu wako boss, mimi ni shabiki wako mkubwa, endelea kutu-inspire, Scott akamjibu.. tafadhali naomba usipost beat zangu ukajidai ni wewe umezitengeneza.

Scott  na chriss & Fat Joe
Baada ya hapo Lamar alimjibu..‘Hakuna matata boss, haitatokea tena‘ na Watanzania wengine wakaanza kucomment akiwemo producer Mtanzania Lucci, wasanii Dogo Janja na Julio Batalia.

Lamar amesema kuwa  baada ya hii ishu na kusema baada ya hizi comments ilibidi amuandikie Scott msg private na kumueleza kwamba hakuwa na nia mbaya kwa alichokifanya,

 Scott alikuwa mpole na kuelewa nia ya Lamar… akamjibu ‘sawa kaka‘
Moja ya kazi ya Producer Scott Storch

Post a Comment

 
Top