0

Mwishoni mwa mwaka 2015 msanii wa bongofleva Mo Music  hakuwa na furaha kwa sababu alipata taarifa za kushtukiza kutoka Mahakamani Dodoma kwamba anashtakiwa kwa kosa la kushirikiana na mpenzi wake wa zamani kutapeli zaidi ya shilingi milioni 30 za mtu.

Leo February 23 2016 Mahakama ya wilaya Dodoma imemuondolea mashtaka Mo Music aliyekua mshtakiwa wa pili kwenye kesi hiyo ambayo muhusika mkuu ni mpenzi wake wa zamani anaeshtakiwa kwa kutapeli zaidi ya milioni 30 za Mwanaume mwingine ambaye alitajwa kuwa mpenzi wake mpya.

Mo Music alisema mwanaume huyo baada ya kushtukia mchezo wa kutapeliwa akaamini Mwanamke huyo aliyekua mtangazaji wa Radio, amekua akichukua pesa kwake na kuzipeleka kwa Mo Music (mpenzi wa zamani)

Mo Music amesema kila ambapo amekua akitaka kutoa wimbo mpya Mwanamke huyo amekua akimletea mabalaa japo tayari ameshaachana naye kitambo, kipindi cha nyuma aliwahi kuzusha kwamba anao ujauzito wa Mo Music na mwanamke huyo alilivalia njuga hili swala mpaka likafika kwenye vyombo mbalimbali vya habari na Mo Music akaamini kachafuliwa jina.

Post a Comment

 
Top