Rapper Nay wa Mitego kupitia akaunti yake ya instagram amepost picha ya sanamu la mimba kama inavyoonekana hapo chini na kuandika

“Eti jamani ivi zinauzwa shillingi Ngapiiiiiii?! #ShikaAdabuYako nitumie kipande unacho kipenda zaidi #ShikaAdabuYako“
Post hiyo imekuaje masaa kadhaa baada ya Idriss kupost kwamba mimba ya Wema imetoka na bila shaka Nay wa Mitego amepata pa kukazia ile diss yake aliyoitoa kwenye wimbo wake wa Shika adabu yako ambapo alimwonya Wema kuwa ana mimba kweli ama anatafuta kiki.
Hii ni post aliyoiandika Mwigizaji Wema Sepetu saa kadhaa baada ya Baba Watoto mshindi wa Big Brother Africa Idris Sultan kuthibitisha kwamba ujauzito huo wa mapacha umeharibika.

Ni kweli, na imeniuma sana lakini kwenye hatua maishani mwangu naweza kusema Alhamdulillah kwa kila kitu, Alhamdulillah kwa wote wanaojua uchungu nilio nao na wameonyesha moyo wa kibinadamu, nawashukuru kwa upendo wenu.. MNANIPA NGUVU.
Alhamdulillah kwa wote wanaojua uchungu nilionao na wamefurahia kwasababu zao binafsi. Nawashukuru kwa uwepo wenu, MNANIPA UJASIRI, Alhamdulillah kwa siku ya kesho Ilimradi nina pumzi, SITACHOKA KUJARIBU TENA.
Post a Comment