Ripoti za msiba zilianza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii kwa baadhi ya mastaa wa filamu na Muziki nchini, kuhusiana nataarifa ya kufariki kwa mmoja kati ya wachekeshaji maarufu nchini Tanzania, Mohammed Abdallah (Kinyambe) kutoka kwenye maigizo ya Vituko Show.
Akizungumza mmoja kati ya wasanii wanaounda Chama Cha Wasanii Wachekeshaji Tanzania, Mkono Mkonole, amesema Kinyambe amefariki jana akiwa mkoani Mbeya.
“Kinyambe alikuwa anasumbuliwa na uvimbe tumboni kwa muda mrefu, ila jana ndo amefariki akiwa mkoani Mbeya, katika hospitali ya mkoa wa Mbeya,” alisema Mkonole.
Kuhusu taratibu za mazishi, Mkonole amesema bado hawajapanga kwani taarifa za kifo chake wamezipokea jana usiku.
“Kusema kweli bado hatujapanga kuhusu mazishi, lakini sasa hivi tunawasiliana na ndugu zake ili kujua taratibu za mazishi na zikamilika tutaweka wazi,” alisema Mkono.
Post a Comment