Diamond akanusha kumsaliti Zari na model wa video ya Raymond ‘Kwetu’
Super star Diamond Platnumz amekanusha tetesi zilizowahi kuvuma mtandaoni kuwa alimsaliti mpenzi wake Zari na mrembo aliyetumika kwenye video ya wimbo wa msanii wake Raymond, Kwetu alipokuwa ajizungumza na fahamu tv.
“Sio kweli, wanahisi hivyo kwasababu ni binti mzuri, wanaamini kwamba kwasababu ni binti mzuri naweza kufanya chochote, kwasababu naonekana kuwa ni maarufu na nina uwezo, Raymon ndio msanii wetu so labda ningeonekana kuwa naweza kuchukua majukumu hayo,” Diamond aalisema.
Tetesi ambazo bado zinaendelea kuvuma zilisababisha msichana huyo aitwaye Irene atukanwe na baadhi ya mashabiki.
Post a Comment