0
Justin Bieber akiwa ameshafanya ziara nyingi kwa ajili ya album yake ya mwisho”Purpose”, pia alikua anatamani kupanua ziara hizo ikiwa pia ni kutembelea nchi kama Argentina lakini yeye pamoja na wafuasi wake wameamua kua kwenda kufanya ziara nchini humo kutaleta matatizo..kwa mujibu wa chanzo cha TMZ kiligundua hilo.
Imeelezwa kua ziara yake ya “purpose” imeleta mafanikio makubwa sana kwa msanii huyo, ikiwa pia Justin Bieber ameweza kutanua ziara hiyo kwenda miji mingine kama America ya kusini, Japan na Australia. 
Lakini swala la kwenda kufanya ziara nchini Argentina ndo limekua la utata, kwasababu hakimu wa nchi hiyo hapo mwanzoni alishawahi toa amri ya mwanamuziki Justin Bieber kukamatwa na kuumuliza zaidi maswali juu ya kesi ya jinai iliyofanywa na moja ya walinzi wake.

 Justin Bieber anahofia kua hakimu huyo anaweza mkamata tena kwa ajili ya kesi ile ile.
Kitu ambacho kinaweza badilisha mawazo ya Justin Bieber , ni kama tu hakimu atatoa tangazo la kuweka wazi uhuru wa mwanamuziki huyo na kumruhusu kurudi nchini humo bila kua na woga wa kukamatwa kwa ajili juu ya kesi hiyo kama ilivyo kua hapo alawali.

Post a Comment

 
Top